Uongozi Wa Kiroho

Ujumbe wa sasa na wa mwisho kutoka kwa Uongozi wa Kiroho unaonekana hapa chini na zinaonekana kwa rangi ya Majenta. Wakati ujumbe mpya ukiwasili Ujumbe wa zamani unahamishiwa kwenye ukurasa wa Ujumbe.

 

1 Octoba 2019

Ni fursa kubwa kwangu kukuandikia ujumbe huu kutoka kwa Uongozi wa Kiroho.

Sisi, katika Ulimwengu wa Kiroho tumeunganishwa na wewe wakati huu maalum sana.

Kuwa na wengi wenu kiasi hiki Walioanzishwa pamoja katika eneo lenye baraka kweli ni hatua kubwa katika Uamsho wa Kiroho wa Sayari ya Dunia. Yaani, Dunia kama Kiumbe na wakazi wake wote.

Hasa Tumevutiwa sana na Upendo na Furaha inayopatikana kutoka kwenye mioyo yenu kwenda kwa kila mmoja wenu na kwa ulimwengu kwa jumla.

Bado kuna maeneo mengi ambapo kuna vita, njaa na magonjwa. Tungependa kuwaomba nyinyi wote kuzingatia kupeleka Upendo wenu kwa umoja katika maeneo haya, kujaribu kufuta migogoro, kuponya wagonjwa na kulisha wanaokufa na njaa.

Kadri watu zaidi na zaidi wanahisi mwito wa Uamsho wa Kiroho, Upendo na Mwanga utashinda Giza kwenye Maeneo haya.

Maelfu ya watu mnapotahajudi kwa pamoja, kweli mtaleta mabadiliko.

Kila kitu kimeunganishwa na Nguvu ya Mwanga itaangaza na kuchomoza.

 

Agosti 1, 2019

Hii ni kutoka kwa Mabwana wa Mwanga, kujibu swali lako toka moyoni.
Sisi katika Ngazi za Kiroho tunaangalia wakati wote na hakuna kitu kinachotokea au kupita bila kutambulika, kama tulivyosema hapo awali.

Tangu mwanzoni wakati Mwanadamu alipomtafuta Muumba wake, imekuwa utafutaji wa ndani wa kiroho, kwa nia safi. (mara nyingi ikitanguliwa na mtikisiko wa ndani wa maisha na maumivu, ya kimwili au vinginevyo)

Utafutaji huo wa ndani, mwishowe, ghafla bila kutarajia ulimwonyesha mtafutaji wa Ukweli Chanzo chake – Umoja wa Vitu vyote. Hii ilikuwa nadra sana.

Kadri muda ulivyoendelea, mambo yalibadilika na mchakato wa Uanzishwaji (Initiation) ukaanza – kufanya mambo yaendelee Kiroho – kuwaongoza watu kwa “kuwaonyesha Mwanga” na kuwaongoza kwenye Safari ya Kiroho, ambapo ndipo tulipo sasa.

Katika siku zijazo, Tungependa kuona kuwa kadiri watu wanavyoendelea kukua na kubadilika kuwa Viumbe wa Juu, wakati ‟Ascension” inavyokomaa, watu watarudi kwenye Kujitafuta wenyewe, lakini kwa uelewa wa ndani zaidi wa “Roho” na mahali na wajibu wao kama Binadamu . (kuwa wamekua (Evolve) zaidi kabla ya kuanza Kutafuta) Itakuwa aina ya ‟Gnosis” ambayo imepenyeza na kuenea ndani ya Nafsi zao.

Kuna wale ambao tayari hufanya hivi na tunatumaini kwamba wakati Mwanga unapotembea na kuzunguka katika giza la udongo (matter), basi Nafsi zaidi na zaidi ‟zitachukuliwa” na Nguvu hii mara moja bila kutegemea kama zamani. Lakini tofauti itakuwa, ni kawaida na sio nadra.

Hii Tunarahisisha – lakini kwa kweli ni ngumu zaidi.

 

Septemba 24, 2019

Hii ni kutoka kwa Mabwana wa Mwanga

Kuwa na imani kwako mwenyewe. Hii ni muhimu kwa sababu, wakati Ascension inakaribia lazima utambue kuwa hakuna mtu yeyote muhimu zaidi kuliko mtu mwingine. Kila mtu ana sababu yao ya kuwa Duniani kwa wakati huu, kama ilivyo pia kwa kila kiumbe.

Hakuna kitendo ambacho ni muhimu zaidi kuliko kingine, hii ni ngumu kuelewa, kwa sababu ili kuona kwamba ni kweli lazima utoke nje ya Ulimwengu utazame nyuma. Kila kiumbe kina kazi yake maalum au jinsi ya kuwa.

Kwa hivyo, unapoamka asubuhi, fikiria siku yako kuwa imejaa Upendo, Kupenda na Kujifunza. Usiku, unapofikiria juu ya siku nzima, jiulize, kwa ujumla, unafurahi jinsi siku ilivyokwenda. Ikiwa sivyo, kwanini?

Kinachofanya siku nzuri kwa mtu mmoja ni tofauti na mtu mwingine. Watu wengine wanahitaji kujaza wakati wao na vitendo; wengine wana nafasi za kutafakari, kuchukua muda na kupumzika. Unaunda ukweli wako mwenyewe.

Suala zima ni kuwa na Kiasi na Uwiano, kama Tulivyosema hapo awali

 

17 Septemba 2019

Hii ni kutoka kwa Mabwana wa Mwanga kuhusu Kutoa

Hakuna chochote Duniani ambacho kwa kweli ‘ni cha’ mtu yeyote. Hiyo inamaanisha ingawa kutoka katika umri mdogo sana watu hufundishwa kuwa hiki, au kile ni chako sivyo ilivyo.

Wewe unakopa tu au unakopeshwa tu vitu kwa wakati uponaishi hapa Duniani. Hii inaweza kuwa dhana ngumu kuelewa lakini ni dhana ambayo ni muhimu sana kuelewa.

Wakati watu zaidi na zaidi wanaelewa kuwa hawamiliki kitu chochote basi wanakuwa wakarimu zaidi..

Mara nyingi utaona kuwa watu wakarimu sana ndio ambao wanacho kidogo zaidi cha kutoa. Hii inaweza kuonekana kuwa kitu cha ajabu na kushangaza hadi utakapogundua kuwa watu hawa mara nyingi ndio wenye furaha zaidi. Watu wenye furaha kwa ujumla ni wakarimu zaidi.

Kuwa na utajiri mkubwa kwa kweli huleta majukumu yake yenyewe, kujitahidi kutunza utajiri huo kunaweza kusababisha wasiwasi na baadaye magonjwa.

Kadiri unapojaribu zaidi kushikilia kitu, ndivyo unavyohisi unakiachia na unakipoteza.

Uwiano na kuwa na Kiasi ndio ufunguo.

 

7 Septemba 2019

Huu ni ujumbe kutoka kwa Mabwana wa Mwanga kwa wote wanaotafuta Hali ya Kiroho, kwa wale ambao wamepokea Mwanga na Sauti na wale ambao wamepata Enlightenment.

Wakati watu wanapoanza kuelewa kuwa kuna kusudi kubwa la maisha kuliko kuishi tu, maisha yao hubadilika kwa kuangalia karibu yao na kuona, labda kwa mara ya kwanza, kwamba kuna uzuri katika mazingira yao ambao walikuwa hawajauona kabisa.

Daima kuna uzuri unapatikana ikiwa mtu anaangalia kwa nguvu za kutosha. Inaweza kuwa ua, au mti, au mtu anayesema ‘habari’ ambaye kwa kawaida alikuwa kama hakutambui.

Mara tu mtu, au kikundi cha watu wanapoanza kugundua uzuri katika vitu, au watu, basi jambo la kushangaza ni kwamba uzuri huanza kukua katika hali isiyo ya kawaida. Ghafla maisha yao hubadilika kutoka kwa uwepo wa kipekee sana na wa tamaa za kibinafsi hadi kukubalika kwa kila kitu na vitu vyote, kama vilivyo, bila kuhukumu.

Hii kawaida inaweza kuchukua miaka mingi, lakini sio lazima ichukue muda mrefu.

Wakati mtu anatembea katika Njia ya kuelekea kwenye Enlightenment, inawezekana kubadilika haraka sana, kwa sababu unagundua kuwa unapohukumu kitu chochote, unajihukumu mwenyewe.
Wakati uzuri wa ndani unapogundulika na kweli kutambulika, basi uzuri wa nje hugundulika pia.

Fikiria ni Uhuru kiasi gani unaopatikana. Kweli Uzuri uko kwenye jicho la mtazamaji.

 

 

Uongozi wa Kiroho ni Nani?

 

Ili sisi tuelewe ni nani au ni nini Uongozi wa kiroho, tunahitaji kwanza kuangalia katika siku za nyuma. Historia inatuonyesha kwamba elimu ya Kiroho ilikuja duniani kwa njia ya walimu wakubwa, mystics, gurus na mara nyingi kuishia kama dini.

Kwa bahati mbaya – Ukweli mara nyingi ulibadilishwa au kupotea kutokana na kiburi (ego), uchoyo, tamaa ya mamlaka n.k.

Tunajua kidogo sana kuhusu Uongozi wa Kiroho licha ya kwamba ni idadi kubwa ya Viumbe “Intelligent” ambao wanaishi kwenye Ngazi za Juu za maumbile (au “Mbinguni” kama ukitaka).

Ngazi hizi za Juu zipo zaidi ya 3 ambazo sisi, kama binadamu, kwa kawaida tunazifahamu kwa hisia zetu ndogo zenye mipaka. Wao ni pamoja na “Masters” waliopaa “Mbinguni” na Viumbe ya Mwanga ambao mara nyingi hujulikana kama Malaika na Viongozi. Wao siku zote huwasiliana nasi, ushahidi mkubwa umerekodiwa katika maandiko yetu, tangu mwanzo wa wanadamu.

Kama tukiangalia kuzuka na kupanda kwa ustaarabu mkubwa tunaona kwamba watu walipata elimu ya ajabu. Maarifa na elimu hudhihirishwa na sanaa, fasihi, teknolojia na sayansi; Chanzo chake ni Uongozi wa Kiroho. Wao waliweka mawazo katika akili za wale waliokuwa tayari kupokea. Mara baada ya wazo kupandikizwa watu wengine wengi wakawa wazi na wakasaidia kuliendeleza.

Kama Elimu ya Kiroho, wakati wazo jipya linadhihirika siku zote kuna watu wanataka kulitumia kwa faida zao binafsi, madaraka na uharibifu. Na hivyo ustaarabu wowote hatimaye huanguka na sehemu kubwa ya maarifa na elimu kupotea.


“Ukweli unapokuwa kwenye kina kirefu sana
Chini ya miaka elfu ya usingizi
Wakati unahitaji, mabadiliko
Na kwa mara nyingine Ukweli unapatikana”

(George Harrison)

 

Leo

Katika miongo michache iliyopita Uongozi wa Kiroho wamewasiliana na walimu wengi wa Kutahajudi duniani kote na kutoa ujumbe mmoja. Sayari yenu pamoja na wakazi wake ni wagonjwa; tunahitaji wewe kuonyesha Ukweli kwa idadi kubwa ya watu. Kama mkifanikiwa basi tunaweza kuinua Ufahamu wa Binadamu. Tunaweza kuwapa teknolojia ya hali ya juu ili kuweza kuboresha maisha yenu ya kimwili. Zaidi ya hayo tunaweza kuwaonyesha Ujuzi mkubwa ili kuchochea akili zenu na kuwasaidia kuelewa nafasi yenu kwenye Ulimwengu (Universe).

The remit is usually the same; Wanataka mtu 1 katika kila watu 100,000 awe amepata Initiation kwenye Mwanga na Sauti ya Kiroho. Basi leo tunavyokaribia idadi ya watu bilioni 7.5 duniani tunakuwa na lengo la watu 75,000.
 

Njia

Kwa wakati huu tunaambiwa kuwa ni muhimu kuwa Elimu ya Kweli ya Kiroho iwafikie watu wote. Hivyo ni lazima kujifunza kutokana na historia na kuhakikisha kama iwezekanavyo kwamba elimu hii inapatikana na mafundisho yanakuwa wazi kabisa.

Hii haitakuwa Safari kwa wachache waliochaguliwa lakini “Enlightenment” kwa ajili ya umma. Wengi wenu hamtajichukulia kuwa watu wa Kiroho lakini kama mmewahi kuhoji kuwepo kwenu, kuwa kwenu au kuhisi ndani ya moyo kuna sehemu inakosekana basi Njia hii ni kwa ajili yenu. Kinachohitajika tu toka kwenu ni kujifunza mazoezi ya kutahajudi, kuwa na maisha ya afya na muhimu zaidi kujifunza jinsi ya kutoa kweli.

Kama ilivyoelezwa hapo juu tunaamini kwamba Uongozi wa kiroho wako nyuma ya Masters wote na Dini ambazo zilishawahi kujulikana duniani. Waliwajibika kwenye ujenzi wa Piramidi, kupanda kwa ustaarabu mkubwa na mafanikio katika sayansi ya kisasa. Wengi watashuhudia kuwepo kwao kama manabii, waonaji, (mystics, clairvoyants) na watu walio na flashi za uvuvioa au ubunifu, na kama wakiwa waaminifu na bila kuwa na ego watashuhudia kuwa haikuwa wao: “Nilikuwa tu nalazimika” au “mawazo yaliaendelea kunijia katika kichwa changu”.

Mnamo Februari 2015 Uongozi wa kiroho waliwasiliana na baadhi yetu tuliokuwa tumefikia hali ya juu ya Ufahamu wa Kiroho na maarifa muhimu na ufahamu unaotakiwa kuweza kutoa Nguvu za Mwanga na Sauti. Tunapenda kufanya kazi kama Uongozi wa Kiroho wanavyofanya, tukiwa nyuma ya “pazia”, sio mbele na kuwa na shirika kubwa na tumeahidi kujitolea maisha yetu kwa Njia hii ya ajabu. Tumeshangazwa na mambo ambayo tumejifunza na tunanyenyekea kwamba tumeteuliwa kutoa Maarifa na Hali za Ufahamu wa Kiroho. Kwetu sisi hakuna heshima, dhumuni au kusudi zaidi inayowezekana kuwepo.

Moja ya makosa makubwa ni kutoza fedha kwa ajili ya Hali za Kiroho; ni chanzo cha kuanguka kwa makundi mengi. Ndiyo maana sisi kamwe hakuna malipo ya kitu chochote na tumechagua sera ya “Kulipia Baadaye” au (“Pay it Forward”).
 

 

Kutoka kwa Uongozi wa Kiroho

Mawasiliano yote ni neno kwa neno, isipokuwa masahihisho ya spelling na vituo vinavyoongezwa inapohitajika. Ujumbe wa awali unapatikana katika ukurasa wa Mawasiliano.

Tunapoangalia kinachoendelea duniani kote sasa hivi, sisi tunakuwa na Matumaini kuwa ni dhahiri zaidi kwamba mambo yanasonga kwenye mwelekeo sahihi. Kuna njia ndefu mpaka kufikia lengo, lakini sisi tunafurahishwa kuona Positivity na Furaha ambayo imekuwa inayofanywa na wale wanaojiandaa na kufungamana na Lightwave mpya na kufikia Hali za Juu katika muda mfupi sana.

Hawa ni Mashujaa wapya ambao wote wana uwezo, ujasiri na Upendo wa kuchukua Nguvu hii ya ajabu na kuleta maelfu ya watu. Wao itakuwa zamu yao kuweza kutoa Upendo waliopata kwa Dunia.

Kutoka kwetu Uongozi wa Kiroho:
Sisi tunaangalia chini na kuridhishwa sana kuwa mmeweka tovuti mpya kuwa tofauti na zingine.

Tuna nia ya kutoa ujumbe, kuweka sasa, mara kwa mara na Tunahisi kwamba ndicho watu wanachotaka na cha kuwahamasisha.

Kutakuwa na watu wengi hivi karibuni watakaoleta chini ujumbe kutoka kwetu kwa lugha nyingine ambazo zina haja ya kuwa na nafasi. Tuna uhakika kwamba hizi tovuti zitakubalika na wengi.

Sisi, Mabwana wa Mwanga, tunahitaji kuwasiliana na kuwasilisha baadhi ya maneno kwenu wote.

Imeandikwa katika vitabu vingi, kwamba kielelezo cha Mwisho cha Mungu, ni Upendo. Na katika mafundisho ya Lightwave mpya, sisi tunasema kwamba, Upendo ni msingi wa kila ujumbe tunaotuma. Ni kwa sababu ya Upendo wetu kwenu, kwamba sisi tunatuma Nguvu na ujumbe wa kuwasaidia Wanaadamu.

Tumeridhika sana kuona kwamba watu wapya Walioanzishwa (waliopata Initiation) wanataka kutoa Upendo huu pia; kwa kila mmoja wao, kwa marafiki na familia na kwa watu wanaofanya kazi bila kuchoka, ili kuhakikisha ustawi wao wakati wa mchakato wa Initiation na kwingineko zaidi.

Ni kwa kueneza Upendo huu tu, pamoja na Huruma na kuelewa, kutafanya Ufahamu wenu kuongezeka hadi kufikia mahali ambapo Dunia itakuwa sehemu nyingine kabisa. Mahali ambapo watu watakuwa wanaangalia kile kilicho Kizuri katika kila mtu na kila kitu.

Hii inaweza kufikiwa sasa hivi!

 

Tahajudi Ya Mwanga na Sauti

Kama kile kilichoandikwa hapo juu kinaoana nawe kwa namna yoyote ile, basi angalia tovuti yetu kuu kwa kubonyeza kiungo hapo chini.

swahili.lightandsoundmeditation.com
www.lightandsoundmeditation.com