Kujifunza Masomo ya Maisha

 
Tunaambiwa kuwa lengo la maisha hapa Duniani ni kujifunza masomo. Haya yanaweza kuwa yenye asili ya kiakili lakini muhimu zaidi ni yale tunayojifunza kwa mahusiano na watu wengine.

Mahusiano wa binadamu ni tata sana na ya aina mbalimbali. Kwa mfano wakati sisi tunashiriki katika baadhi ya shughuli kuna ‘ “watu watatu” wanaohusika, sisi wenyewe, kile tunachofikiria ni sisi na yule ambaye watu wengine wanamuona. Matatizo makubwa zaidi ambayo yanatokea kati ya watu yanatokana na kutoelewana kidogo au tofauti kidogo ya maoni yao.

Unaweza kuangalia tu migongano kwenye familia au vita za kidini na kuona kwamba hii ni kweli!

Vilevile tunaelewa kwamba wakati sisi tunachukua miili maisha yetu kwa ujumla yameshapangwa yatakavyokuwa. Sisi tunachagua wazazi wetu, marafiki zetu, wapi tutaishi pamoja na washirika wetu wa ndoa pamoja na watoto. Ni kana kwamba tuna sehemu katika kucheza mchezo na tunafuata maelekezo.

Hata hivyo, kama ilivyo kwenye michezo wa kuigiza, mwigizaji wakati mwingine anakuwa na mashaka na matatizo juu ya mistari na maelekezo yake na ku”improvise”. Matokeo yake yanaweza kuwa janga kamili au vizuri kabisa. Hapa ndipo utashi huru (free will) unapoingia, tuna uhuru na tunaweza kutofuata mpango wetu wakati wowote tunapotaka, hivi ndivyo tunavyopata Karma (nzuri au mbaya). Kama tukifuata maelekezo ya mchezo na mistari yetu kama ilivyoandikwa basi hatutakuwa na Karma ya kulipia.

Je, sisi tunajuaje masomo yetu? Ingawaje kwa ujumla tunafuata maelekezo ya mchezo hatuna ufahamu wa maelekezo na mistari hii na hatuna ufahamu wa mchezo kwa hivyo hatuwezi kuona nini tunahitaji kujifunza. Hata hivyo, kwa masomo mengi kunakuwa na kidokezo!

Kama tunaona na kupata changamoto au tatizo linalorudia mara kwa mara ni ishara wazi kuwa hili ni moja ya masomo yetu makuu. Jibu rahisi ni kulipokea, kulitatua na kulimaliza. Kama hutalikabili litaendelea kujitokeza mpaka utakapochukua hatua.

Watu wengi wanahangaika katika maisha kwa sababu wao hushinikiza mambo nyuma kwenye mawazo yao bila kuyatatua. Hiyo ndivyo “stress” inavyotokea, wakati “in-tray” limejaa tele. Hivyo ushauri ni kujaribu kutatua mambo wakati yanapoonekana na sio kuyaacha mpaka kesho. Vitendo hutakasa mawazo!

Hatimaye kitendawili cha mema na mabaya. Asili yetu ya kweli ni kwamba sisi sote kwenye Kiini ni Roho; baadhi yetu tunajua hayo, baadhi yetu hatujui. Tunaweza kuzungumza kuhusu mtu mbaya au jambo jema lakini kumbuka katika ngazi hii sisi tunazungumzia juu ya sehemu ya mtu ambayo amechagua kucheza.

Kama mtu anacheza kuwa muuaji katika filamu au mchezo, kwenye mchezo ujao huenda anaweza kuwa mtakatifu! Masomo ambayo muuaji anajifunza bila shaka hayawezi kuwa kama masomo ya mtu mtakatifu, na ya mtu mtakatifu kuwa sawa na ya muuaji.

Kwa hiyo kwa kuwa hakuna hata mmoja wetu kiasili ni mbaya ni busara kuona sifa nzuri kwa watu na katika maneno ya Uongozi Wa Kiroho Kukubali, Kupenda na Kusamehe.

Post navigation