Uongozi unataka kuunganisha uwezo wetu wa Kutahajudi kutuma Upendo kwenye Sayari. Njia hii ni sawa na utumaji wa Nguvu za kuponya ambazo baadhi yenu huenda tayari wanafanya.
Mchakato huo ni rahisi na wa kutosheleza. Jaribu kufanya utoaji wa Upendo kuwa sehemu ya mazoezi yako ya kutahajudi kila siku.
Kaa kwa faraja wakati mgongo umenyooka kuelekea juu vizuri na weka mikono pemdeni usawa na mapaja, na viganja vikielekea juu. Kisha, ukiwa umefunga macho, kuwa na mtazamo na kuunda nia; hii inaweza kupatikana kwa njia kadhaa.
Unapaswa kutafuta ni njia ipi inayofaa kwako:
1) kwa kutumia uthibitisho kama “Mimi ni mfereji safi na ninatuma Upendo kwa Sayari.” Hii lazima irudiwe mara chache mpaka unahisi Nishati itokayo kwenye viganja vyako.
2) kwa kutumia taswira, tengeneza picha ya Sayari kama inavyoonekana kutoka angani na hisi kutoka kwenye Moyo wako mtiririko wa Upendo kuilinda na kuikuza, (kama vile ambavyo ungefanya kwa mtoto mchanga).
3) tena kutumia taswira safiri duniani kote na ona katika akili yako maeneo ya uharibifu. Kwa mfano: sehemu zilizoharibika na ukiwa, misitu iliyoharibiwa, maziwa yenye mazingara machafu n.k.
4) zingatia wakazi wa Sayari (sio watu binafsi); tazama mbele yako makundi ya watu wenye huzuni ambao wanakabiliwa labda na njaa, wasio na makazi au waliopoteza wapendwa wao. Tuma Upendo kutoka kwa Moyo wako kuwafariji.
Unapofanya mazoezi ya mbinu hii utakuwa kwanza unahisi Nishati inayotoka kwenye viganja vyako na kisha unavyozidi kufungamana zaidi utasikia mwili wako wote una‟resonate”. Inapaswa kuwa uzoefu wenye kusisimua na mzuri… mfereji wa Utoaji Safi.
Tafadhali jaribu kufanya hii kuwa sehemu muhimu ya kutahajudi kwako na kufanya hivi dakika 5 kila siku. Kile unachopokea ni cha thamani sana; kwa kutuma Upendo kwa Sayari unaonyesha shukrani yako na shukrani kwa Uongozi ambapo Nguvu zote zinatoka. Ni njia ambayo unaweza kusema Asante.
Kadri idadi yetu inavyokua zaidi na zaidi watu watashiriki katika shughuli hii na nguvu yake itaongezeka kwa kiasi kikubwa. Kila mtu anaye Tahajudi ana sehemu muhimu ya kufanya … .usipoteze Nguvu uliyonayo … unaweza kuleta tofauti halisi.
Wakati idadi ya watu walioanzishwa (Initiates) ikifikia lengo lake tunauambiwa athari yake itaongezeka kwa kasi. Hebu fikiria maji yaliyotembea kwenye mabomba ya bwawa kubwa, halafu siku moja shinikizo la maji nyuma ya bwawa kuvunja kwa njia ya kusafisha kila kitu katika njia yake. Kwa bidii na kazi ngumu upande wetu na kwa msaada wa Uongozi tutatengeneza wimbi la Nishati ya kutakasa ambalo litaenea Duniani kote na kurejesha uwiano na maelewano ambayo yanahitajika sana wakati huu.