Watu wengi wamekuzwa katika familia ambazo ni washiriki wa kanisa au kikundi cha dini. Tangu wakiwa na umri mdogo wanafundishwa nini cha kuamini na kutoamini. Hii si lazima kufanyika kwa makusudi; ikiwa kila mtu anayekuzunguka unafikiri kwa namna fulani ni ngumu kuwa mkweli na mwadilifu na kuendeleza mawazo yako mwenyewe.
Dini nyingi pengine zilizuka wakati wa Kweli. Kwa mfano, Biblia ya Kikristo inasema juu ya Ubatizo wa Yesu ambao unaweza kutafsiriwa kama ubatizo au uanzishwaji wa Kiroho (Spiritual Initiation). Itakuwa na maana kamilifu kwamba Yesu alipata nguvu za Mwanga na Sauti baada ya hapo alitumia siku 40 usiku na mchana jangwani ili kufikia Enlightenment. Katika kipindi hiki alipipambana na akili yake ambayo inajulikana kwa kila mtu anayejaribu kutahajudi (meditate). Ilikuwa tu baada ya matukio haya mawili ambapo alianza kufundisha!
Kufuatia kifo chake wanafunzi wanaweza kuwa walikuwa na uwezo wa kupitisha na kuwafunulia Nguvu hizi watu wengine lakini inaonekana kuwa baada ya muda nguvu zilipungua. Badala yake, ufunuo ulibadilishwa kuwa sherehe na dogma na mkazo ukawa kwenye imani badala ya ugunduzi wa kibinafsi. Haikuwa muda mrefu baadae majengo yalijengwa na pesa ilitakiwa kuhakikisha wokovu wa mtu binafsi. Ni ajabu kutambua kwamba mpaka hivi karibuni Biblia ilikuwa inapatikana tu kwa Kigiriki na Kilatini.
Ni muhimu kwamba tunapoanzisha watu Kutahajudi na kuzungumza juu ya Mwanga na Sauti tunaelezea kwamba wanahitaji kupata Ukweli wao wenyewe. Maarifa yetu sio Maarifa yao, Ufahamu wetu sio Ufahamu wao! Sisi tupo tu kuwasaidia na kuwaongoza. Hakuna haja ya imani. Njia bora zaidi ni kuwa na uchunguzi tu pamoja na kuwa na moyo wazi.
Mwanga na Sauti ama ipo au haipo … ni kwa Mtafutaji kutafuta kipi ni kweli.