Ushuhuda (K.K.)

 

Kuna hii Nishati ambayo inapotumika vizuri au wakati wanadamu wakiwa chini yake na kuoanishwa nayo kwa njia sahihi inatoa uwezo wa kusafiri kwenye Ngazi na Vipimo vya Juu.

Nikiwa katika ya Viumbe wengi ghafla nilikuwa na utambuzi wa ngazi ya maumbile ambayo kwa kawaida sikuwa na ufahamu wake. Wakati nachunguza ukweli niligundua kuwa viumbe wengine walikuwa na ufahamu wa ngazi hii lakini sio wote.

Ilikuwa kama vile picha ambayo muda wote ilikuwa ukutani ghafla imekuwa hai na viumbe wote waliopo kwenye picha ile wamekuwa hai na kila kitu kilikuwa cha kusisimua sana.

Ngazi hii ya maumbile ilikuwa imejaa Viumbe ambao hukaa hapo na kwa ukaguzi wa karibu viumbe hawa walionekana hawana hatari lakini walikuwa na udadisi kuhusu mimi. Katika kile nilichokiona kama udadisi wangu kwa viumbe hawa nilipuliza hewa taratibu kwa upole kutoka kinywani mwangu na ghafla viumbe waligeuka kuwa chembechembe ambazo zilitoweka ndani yangu.

Mara nyingine ngazi ileile tena na wakati huu ninaonekana kuwa ninaelea ndani yake na nikatambua kuwa kulikuwa na Viumbe na kwamba hii yote iko ndani yangu. Ninavyoendelea kuelea kwenye ngazi hii ya maumbile nakutana na Kiumbe ambaye amepata ukombozi wa Ufahamu wa Kiroho (Enlightened Being) ambaye alinikumbatia kwa ukarimu sana na UPENDO mwingi.