Taswira ya Upendo

 
Ngazi hii ya maumbile ya kimwili imejaa madhihiriso na maonyesho mazuri tunayoyaona tunapo‟vibrate” kwa hali ya juu. Leo nilisikia kuhusu mashambulizi ya kigaidi. Watu huzungumzia mashambulizi na hujazwa na chuki dhidi ya washambuliaji. Wanaongea hivyo kwa sababu wanaogopa. Hofu inaunganisha washambuliaji na waathirika pamoja. Kama tukitazama kwa upeo zaidi, mateso na maumivu yanayosababishwa na chuki na hofu hayajaanzia Ulaya, yamekuwa kila mahali katika sayari kwa muda mrefu na wanadamu wamelala kutokana na tamaa ya madaraka.

Wakati ukatili unafanyika karibu yetu, ‟vibrations” yetu hupungua kwa sababu ya kujisalimisha kwa hofu kwa niaba ya wapendwa wetu. Hebu tuinuke juu na kupanua na kueneza Upendo, na Upole ambao ulituleta kuwepo. Tunaweza wote kukumbuka kuwa sisi ni nani. Wewe unayetahajudi na kuona zaidi, jaribu kuwa na taswira na madhihirisho ya Upendo Duniani. Hebu tufanye wote pamoja, kwa sababu sote tumeunganishwa.
(Y.F.)