Uongozi wa Kiroho ni Nini au Nani hasa?

 

Uongozi wa Kiroho ni jina tunalowapa Viumbe wengi wasio na idadi wanaoishi katika Vipimo vya Juu au ngazi za juu za Ulimwengu. Baadhi, lakini sio wote, wamekuwa na maisha ya hapa duniani na wakati mwingine hujulikana kama ‟Ascended Masters”. Baadhi ya Viumbe hawa wanayo mawasiliano na watu Duniani kote. Mawasiliano hutokea kwa kawaida wakati mtu anatahajudi lakini pia yanaweza kutokea wakati wa shughuli za kila siku.

Mtu anayepokea ujumbe atakuwa na ufahamu wa Uwepo na “Sauti” ndani ya kichwa chake; hii inaweza pia kuambatana na aina fulani ya kitu cha kuonekana. Maono haya kwa kawaida yatakuwa ya kibinadamu katika asili ambayo inaweza kuwakilisha mwanaume au mwanamke. Tunaambiwa kwamba wanaunda picha kama hiyo ili kukubalika kwetu; Inaonekana wanatuona na wanatutambua kama mkusanyiko wa Mwanga!

Ujumbe zina mandhari moja ya pamoja, na ni kusaidia Sayari hii na wakazi wake na viumbe hai. Sisi kama wanadamu tumeitumia Dunia sana kuliko inavyopasa na ni muhimu kwamba “tuamke” na kuchukua hatua za kurekebisha.

Kikundi chetu kinalenga kwenye Ufahamu wa Binadamu na maendeleo yake kwa kutumia kutahajudi kwa nguvu ambazo ziko katika hali ya juu ya Kiroho. Tumepokea kiasi cha ajabu cha uongozi kutoka kwa Uongozi wa Kiroho na Wao wanawajibuka kwa kuanzishwa kwa Njia hii na ukuaji wake Duniani kote.

Kadri watu zaidi na zaidi wanavyofahamu Nguvu za Mwanga na Sauti ndivyo wanavyotambua Kweli kuhusu Elimu ya Kiroho. Haipatikani katika falsafa au dini, haiwezi kufundishwa au kufungwa katika kitabu, inaweza kupatikana tu ndani yetu. Ni zaidi ya mawazo na dhana zote; ni Asili yetu tu ya Kweli na kila mtu anahitaji kuigundua mwenyewe.

Uongozi wa Kiroho unatoa kiasi kikubwa cha Nishati kusaidia katika mchakato huu. Hii imesababisha watu kuanza kusikia sauti za hali ya juu na wengine wanaona Mwanga mzuri wa Ndani.