Uongozi Wa Kiroho

 

Umeongozwa kuja kwenye tovuti hii….Hakuna kinachofanyika kwa bahati!

Ujumbe wa sasa na wa mwisho kutoka kwa Uongozi wa Kiroho unaonekana hapa chini na zinaonekana kwa rangi ya Majenta. Wakati ujumbe mpya ukiwasili Ujumbe wa zamani unahamishiwa kwenye ukurasa wa Ujumbe.

 


Ujumbe Wa Mwaka 2024

1 Januari 2024

Salamu kwenu wote kutoka kwa Mabwana wa Mwanga.

Ni kwa furaha kubwa kwamba Tunakuja na Ujumbe wa Mwaka Mpya wakati mwaka wa 2024 unapoanza.

Mwaka Mpya unaashiria mwanzo mpya, kila mwaka una matatizo na vivutio vyake na mambo muhimu, iwe kibinafsi na kimataifa.

Ascension sasa inaendelea katika awamu yake inayofuata, hii imekuwa ikitokea kwa muda, lakini itatambulika kikamilifu kama athari zinaanza kuonekana katika jamii.

Tumetuma zana nyingi kuwasaidia, kuwaongoza, kuwaponya na kuwafundisha. Zana hizi zitakuwa muhimu sana, hasa katika nyakati zijazo, mnapokabiliana na changamoto. Kuna mabadiliko makubwa mbele!

Kama tulivyotangulia kusema, usifiche Mwanga wako; ukiona watu wana shida tumia Upendo na Mwanga wako kuwaonyesha njia. Ukiona watu wanasitasita kubadili njia za zamani waongoze kuona njia mpya. Yote yanahusiana na kuacha mambo yote ambayo si ya lazima katika jamii ya leo. ni wazo zuri la zamani la kuachilia njia za zamani za tabia na kufikiria, na kukumbatia njia ambazo zingeonekana kuwa kali hapo awali. Mfano wa hili ni kutafuta njia za kujiponya badala ya kutegemea wataalamu waliokithiri, hata dawa mbadala!

Amini katika Nguvu ya Mantras.
Amini katika Nguvu ya uponyaji kutoka kwenye Ngazi zigine za Maumbile.
Amini katika Nguvu yako mwenyewe.

 

 

Uongozi wa Kiroho ni Nani?

Ili sisi tuelewe ni nani au ni nini Uongozi wa kiroho, tunahitaji kwanza kuangalia katika siku za nyuma. Historia inatuonyesha kwamba elimu ya Kiroho ilikuja duniani kwa njia ya walimu wakubwa, mystics, gurus na mara nyingi kuishia kama dini.

Kwa bahati mbaya – Ukweli mara nyingi ulibadilishwa au kupotea kutokana na kiburi (ego), uchoyo, tamaa ya mamlaka n.k.

Tunajua kidogo sana kuhusu Uongozi wa Kiroho licha ya kwamba ni idadi kubwa ya Viumbe “Intelligent Beings” ambao wanaishi kwenye Ngazi za Juu za maumbile (au “Mbinguni” kama ukitaka).

Ngazi hizi za Juu zipo zaidi ya 3 ambazo sisi, kama binadamu, kwa kawaida tunazifahamu kwa hisia zetu ndogo zenye mipaka. Wao ni pamoja na “Masters” waliopaa “Mbinguni” na Viumbe wa Mwanga ambao mara nyingi hujulikana kama Malaika na Viongozi. Wao siku zote huwasiliana nasi, ushahidi mkubwa umerekodiwa katika maandiko yetu, tangu mwanzo wa wanadamu.

Kama tukiangalia kuzuka na kupanda kwa ustaarabu mkubwa tunaona kwamba watu walipata elimu ya ajabu. Maarifa na elimu hudhihirishwa na sanaa, fasihi, teknolojia na sayansi; Chanzo chake ni Uongozi wa Kiroho. Wao waliweka mawazo katika akili za wale waliokuwa tayari kupokea. Mara baada ya wazo kupandikizwa watu wengine wengi wakawa wazi na wakasaidia kuliendeleza.

Kama Elimu ya Kiroho, wakati wazo jipya linadhihirika siku zote kuna watu wanataka kulitumia kwa faida zao binafsi, madaraka na uharibifu. Na hivyo ustaarabu wowote hatimaye huanguka na sehemu kubwa ya maarifa na elimu kupotea.


“Ukweli unapokuwa kwenye kina kirefu sana
Chini ya miaka elfu ya usingizi
Wakati unahitaji, mabadiliko
Na kwa mara nyingine Ukweli unapatikana”

(George Harrison)

 

Leo

Katika miongo michache iliyopita Uongozi wa Kiroho wamewasiliana na walimu wengi wa Kutahajudi duniani kote na kutoa ujumbe mmoja. Sayari yenu pamoja na wakazi wake ni wagonjwa; tunahitaji wewe kuonyesha Ukweli kwa idadi kubwa ya watu. Kama mkifanikiwa basi tunaweza kuinua Ufahamu wa Binadamu. Tunaweza kuwapa teknolojia ya hali ya juu ili kuweza kuboresha maisha yenu ya kimwili. Zaidi ya hayo tunaweza kuwaonyesha Ujuzi mkubwa ili kuchochea akili zenu na kuwasaidia kuelewa nafasi yenu kwenye Ulimwengu (Universe).

Kwa kawaida kiwango ni kile kile; Wanataka mtu 1 katika kila watu 100,000 awe amepata Initiation kwenye Mwanga na Sauti ya Kiroho. Kwa hivyo wakati wa kuandika (2016), tulipokaribia idadi ya watu bilioni 7.5 Duniani tulikuwa tunatafuta lengo la watu 75,000. Hata hivyo, mwaka 2019 lengo lilifikiwa na kusababisha mamilioni ya watu duniani kote kuwa na Uamsho wa Papo Hapo!
 

Njia

Kwa wakati huu tunaambiwa kuwa ni muhimu kuwa Elimu ya Kweli ya Kiroho iwafikie watu wote. Hivyo ni lazima kujifunza kutokana na historia na kuhakikisha kama iwezekanavyo kwamba elimu hii inapatikana na mafundisho yanakuwa wazi kabisa.

Hii haitakuwa Safari kwa wachache waliochaguliwa lakini “Enlightenment” kwa ajili ya umma. Wengi wenu hamtajichukulia kuwa watu wa Kiroho lakini kama mmewahi kuhoji kuwepo kwenu, kuwa kwenu au kuhisi ndani ya moyo kuna sehemu inakosekana basi Njia hii ni kwa ajili yenu. Kinachohitajika tu toka kwenu ni kujifunza mazoezi ya kutahajudi, kuwa na maisha ya afya na muhimu zaidi kujifunza jinsi ya kutoa kweli.

Kama ilivyoelezwa hapo juu tunaamini kwamba Uongozi wa kiroho wako nyuma ya Masters wote na Dini ambazo zilishawahi kujulikana duniani. Waliwajibika kwenye ujenzi wa Piramidi, kupanda kwa ustaarabu mkubwa na mafanikio katika sayansi ya kisasa. Wengi watashuhudia kuwepo kwao kama manabii, waonaji, (mystics, clairvoyants) na watu walio na flashi za uvuvioa au ubunifu, na kama wakiwa waaminifu na bila kuwa na ego watashuhudia kuwa haikuwa wao: “Nilikuwa tu nalazimika” au “mawazo yaliaendelea kunijia katika kichwa changu”.

Mnamo Februari 2015 Uongozi wa kiroho waliwasiliana na baadhi yetu tuliokuwa tumefikia hali ya juu ya Ufahamu wa Kiroho na maarifa muhimu na ufahamu unaotakiwa kuweza kutoa Nguvu za Mwanga na Sauti. Tunapenda kufanya kazi kama Uongozi wa Kiroho wanavyofanya, tukiwa nyuma ya “pazia”, sio mbele na kuwa na shirika kubwa na tumeahidi kujitolea maisha yetu kwa Njia hii ya ajabu. Tumeshangazwa na mambo ambayo tumejifunza na tunanyenyekea kwamba tumeteuliwa kutoa Maarifa na Hali za Ufahamu wa Kiroho. Kwetu sisi hakuna heshima, dhumuni au kusudi zaidi inayowezekana kuwepo.

Moja ya makosa makubwa ni kutoza fedha kwa ajili ya Hali za Kiroho; ni chanzo cha kuanguka kwa makundi mengi. Ndiyo maana sisi kamwe hakuna malipo ya kitu chochote na tumechagua sera ya “Kulipia Baadaye” au (“Pay it Forward”).
 

 

Kutoka kwa Uongozi wa Kiroho

Mawasiliano yote ni neno kwa neno, isipokuwa masahihisho ya spelling na vituo vinavyoongezwa inapohitajika. Ujumbe wa awali unapatikana katika ukurasa wa Mawasiliano.

Tunapoangalia kinachoendelea duniani kote sasa hivi, sisi tunakuwa na Matumaini kuwa ni dhahiri zaidi kwamba mambo yanasonga kwenye mwelekeo sahihi. Kuna njia ndefu mpaka kufikia lengo, lakini sisi tunafurahishwa kuona Positivity na Furaha ambayo imekuwa inayofanywa na wale wanaojiandaa na kufungamana na Lightwave mpya na kufikia Hali za Juu katika muda mfupi sana.

Hawa ni Mashujaa wapya ambao wote wana uwezo, ujasiri na Upendo wa kuchukua Nguvu hii ya ajabu na kuleta maelfu ya watu. Wao itakuwa zamu yao kuweza kutoa Upendo waliopata kwa Dunia.

Kutoka kwetu Uongozi wa Kiroho:
Sisi tunaangalia chini na kuridhishwa sana kuwa mmeweka tovuti mpya kuwa tofauti na zingine.

Tuna nia ya kutoa ujumbe, kuweka sasa, mara kwa mara na Tunahisi kwamba ndicho watu wanachotaka na cha kuwahamasisha.

Kutakuwa na watu wengi hivi karibuni watakaoleta chini ujumbe kutoka kwetu kwa lugha nyingine ambazo zina haja ya kuwa na nafasi. Tuna uhakika kwamba hizi tovuti zitakubalika na wengi.

Sisi, Mabwana wa Mwanga, tunahitaji kuwasiliana na kuwasilisha baadhi ya maneno kwenu wote.

Imeandikwa katika vitabu vingi, kwamba kielelezo cha Mwisho cha Mungu, ni Upendo. Na katika mafundisho ya Lightwave mpya, sisi tunasema kwamba, Upendo ni msingi wa kila ujumbe tunaotuma. Ni kwa sababu ya Upendo wetu kwenu, kwamba sisi tunatuma Nguvu na ujumbe wa kuwasaidia Wanaadamu.

Tumeridhika sana kuona kwamba watu wapya Walioanzishwa (waliopata Initiation) wanataka kutoa Upendo huu pia; kwa kila mmoja wao, kwa marafiki na familia na kwa watu wanaofanya kazi bila kuchoka, ili kuhakikisha ustawi wao wakati wa mchakato wa Initiation na kwingineko zaidi.

Ni kwa kueneza Upendo huu tu, pamoja na Huruma na kuelewa, kutafanya Ufahamu wenu kuongezeka hadi kufikia mahali ambapo Dunia itakuwa sehemu nyingine kabisa. Mahali ambapo watu watakuwa wanaangalia kile kilicho Kizuri katika kila mtu na kila kitu.

Hii inaweza kufikiwa sasa hivi!

 

Tahajudi Ya Mwanga na Sauti

Kama kile kilichoandikwa hapo juu kinaoana nawe kwa namna yoyote ile, basi angalia tovuti yetu kuu kwa kubonyeza kiungo hapo chini.

swahili.lightandsoundmeditation.com
www.lightandsoundmeditation.com