Mwanga

Watu Wanaona Mwanga mzuri wa Ndani

 
Tumetambua kuwa idadi kubwa ya watu wanaanza Kuona Mwanga mzuri wa Ndani ambao hauonekana kuwa wa kimwili kiasili.

Maelezo yao hutofautiana lakini ni pamoja na yafuatayo: vipointi vidogo vinavyon’gaa vya Mwanga kama unaangalia anga ilyojaa nyota, jiometria za kushangaza na usahihi usiyofikirika na kulinganishwa, kitu chenye mwanga usioelezeka ambacho kinafanana na Jua. Katika kila kesi muhusika anabainisha kuwa Mwanga unaonekana kuwa hai, wenye akili na kuonyesha Upendo na baadhi yao hupokea ujumbe kwamba wanapaswa kufuata Mwanga kwenye Safari.

Mwangakwai kawaida huonekana wakati uko kwenye chumba chenye giza mara nyingi tu kabla ya kupata usingizi. Baadhi ya watu walituambia kwamba walidhani chumba chao kilikuwa kimeangazwa na mwanga wa taa za mbele za gari, hata hivyo walipofungua macho yao kulikuwa na giza nene!
Mara baada ya mwanga kuonekana kuna uwezekano wa kutokea tena na mtu anaweza kurudi tena na tena. Baada ya muda kile kinachoonekana kinaweza kuanza kubadilika. Wakati mabadiliko yakitokea yanaweza kuambatana na hisia ya movement ya haraka.

Mwanga upo daima lakini watu hawawezi kuona mpaka kujioanisha na “WimbiMwanga” (Lightwave) ya Nguvu za Kiroho. Ni sawa na ishara ya kwanza ya mwanga ambayo inaashiria mwanzo wa alfajiri mpya. Kwanza mng’ao uliofifia, kisha mionzi inamulika anga la mashariki ikifuatiwa na ukuu wa tufe kali lenyewe.

 


 

WimbiMwanga Jipya (New Lightwave)

 
Tumeambiwa kuwa sababu ya haya kutokea ni kwa sababu ya idadi kubwa ya watu wanaoazishwa (initiations) na Enlightenments ambazo zinatokea kwenye Sayari yote. Haya yamefanyika kutokana na WimbiMwanga Jipya (New Lightwave) ya Nguvu ya Kiroho ambayo imeachiliwa na kutolewa kwa wakati huu, ambayo Nguvu yake haijawahi kutokea kabisa.

Inaonekana kwamba Dunia na sisi wenyewe sio tofauti lakini kiundani tunategemeana. Maslahi yetu kimwili na Kiroho hutegemea hali ya Sayari. Kwa miaka mingi sisi tumepora rasilimali za madini na kuharibu vitu vingi vyenye uhai kupitia uchafuzi wa makazi yao. Ingawa sio wazi, ugonjwa wa Sayari umekuwa na athari mbaya kwetu sisi kama Viumbe Watu. Tumekuwa wayakinifu sana tumepunguza kuwa nyeti kwa ustawi wa wanadamu wenzetu. Kanuni za maadili na harakati za Kiroho zimeanza kutokuwa na kipaumbele kwnye jamii ya “mimi kwanza”.

Hii ilikuwa ndio sababu Njia hili ilianzishwa, kuleta Elimu ya Kiroho kwa watu wote. Kwa sababu hii imesababisha mwamko wa Nguvu wa Sayari; ni kana kwamba inaanza “kuimba”. Hapo awali, mtu angekuwa anahitajika kuanzishwa (Initiation) ili kusikia Sauti lakini sasa idadi ya watu zaidi huwa ni kawaida kuisikia kiasili.

Uliza familia yako, majirani na marafiki kama wanawezi kuisikia. Unaweza kushangaa jinsi ambavyo ni kitu cha kawaida. Wengi watakuwa na udadisi, kama ni hivyo, tafadhali waelekeze kwenye tovuti hii ili kuwasaidia kuelewa Ukweli juu ya hicho walichoona.

Hebu tujulishe ulichosikia; tungependa kujua jinsi hii ilivyoenea na jinsi watu wanavyosema. Ukipenda kututumia barua pepe Bofya Hapa tu.