Sauti Ya Kiroho

Watu Wanasikia Sauti za Mzunguko wa Juu (High Frequency Sounds)

 
Tumetambua kuwa idadi kubwa ya watu (wengi wao vijana) wamekuwa na ufahamu wa sauti za mzunguko wa juu (high frequency) ambazo hazionekani kuwa na asili ya kimwili.

Maelezo yao wote ni sawa kabisa, wanasikia seti ya mizunguko (frequencies), mara nyingi sauti imara kwa nguvu na kasi, ambayo inaweza kuonekana na kutoweka kwa unasibu (randomly). Wanaweza kuwa hata kwenye mazingira yenye kelele lakini kwa kawaida hutokea wakati mtu ametulia, mara nyingi kabla ya kupata usingizi.

Kama ukisema kwa watu wengi wao watasema kuwa hawajapata kusikia sauti hiyo. Hata hivyo, la kushangaza, watu wachache, wanasema: “Ndio !, ghafla imetokea”. Hawakuwa na ufahamu huo mpaka tulipowauliza. Ni kana kwamba tunaweza kwa namna fulani kuwatuni! Mara baada ya kuisikika, wao wanaendelea kuwa na uwezo wa kuipata Sauti.

Tumeambiwa kuwa sababu hii hutokea ni kwa sababu ya idadi kubwa ya watu kuanzishwa (initiations) na Enlightenment ambazo zinatokea kwenye Sayari. Haya yamefanyika kutokana na WimbiMwanga Mpya (New Lightwave) ya Nishati Ya Kiroho ambayo imeachiliwa kwa wakati huu, Nguvu ambayo kamwe haijawahi kutokea.

Sauti daima ipo lakini watu hawawezi kuisikia mpaka wanapojioanisha na WimbiMwanga (Lightwave) ya Nguvu za Kiroho. Ni sawa na “korasi ya alfajiri”; kama mionzi ya kwanza ya jua inapoanza kuangaza anga, ndege wanaanza kuimba wimbo na Asili kuamshwa kutoka kwenye “usingizi” wake.

Inaonekana kwamba Dunia na sisi wenyewe sio tofauti lakini kiundani tunategemeana. Maslahi yetu kimwili na Kiroho hutegemea hali ya Sayari. Kwa miaka mingi sisi tumepora rasilimali za madini na kuharibu vitu vingi vyenye uhai kupitia uchafuzi wa makazi yao. Ingawa sio wazi, ugonjwa wa Sayari umekuwa na athari mbaya kwetu sisi kama Viumbe Watu. Tumekuwa wayakinifu sana tumepunguza kuwa nyeti kwa ustawi wa wanadamu wenzetu. Kanuni za maadili na harakati za Kiroho zimeanza kutokuwa na kipaumbele kwnye jamii ya “mimi kwanza”.

Hii ilikuwa ndio sababu Njia hili ilianzishwa, kuleta Elimu ya Kiroho kwa watu wote. Kwa sababu hii imesababisha mwamko wa Nguvu wa Sayari; ni kana kwamba inaanza “kuimba”. Hapo awali, mtu angekuwa anahitajika kuanzishwa (Initiation) ili kusikia Sauti lakini sasa idadi ya watu zaidi huwa ni kawaida kuisikia kiasili.

Uliza familia yako, majirani na marafiki kama wanawezi kuisikia. Unaweza kushangaa jinsi ambavyo ni kitu cha kawaida. Wengi watakuwa na udadisi, kama ni hivyo, tafadhali waelekeze kwenye tovuti hii ili kuwasaidia kuelewa Ukweli juu ya hicho walichoona.

Hebu tujulishe ulichosikia; tungependa kujua jinsi hii ilivyoenea na jinsi watu wanavyosema. Ukipenda kututumia barua pepe Bofya Hapa tu.

 

 

Ushauri wa Kutahajudi kwenye Sauti

Kama wewe unasikia Sauti za mizunguko ya juu (high frequency) tunapendekeza sana kwamba ujifunze kutahajudi kwenye Sauti hizi. Ulichopewa ni zawadi ya ajabu ambayo kama ikitumika kwa uwezo wake kamili itaonyesha ufahamu mkubwa wa asili yako ya Kweli ya Kiroho.

Unaweza kuwa umesoma kwamba Wahenga Wakubwa na Mayogi katika nyakati zote wametumia Tahajudi kama chombo cha kufungua Siri na kugundua Hali za Furaha ya ajabu, Neema na Enlightenment ya Kiroho. Wao pia walikuwa na ufahamu wa mtiririko wa Sauti na waliitumia kama lengo kwa ndani katika Tahajudi yao.

Sauti hii huelekea kuja na kwenda kana kwamba ina akili yake yenyewe. Jaribu kutafuta mahali fulani pazuri na ukae; hii inaweza kuwa juu ya mto au kwenye kiti. Ni vyema kuweka mgongo wako sawa na kuwa umenyooka kuelekea juu. Lenga ufahamu wako kwa upole kwenye Sauti bila kujaribu kuichambua; iache iwepo tu!

Unaweza kusikia kuwa nguvu itaongezaka na itakuwa ya kina zaidi. Unavyojifunza kupumzika na kujiachia Sauti itaonekana kama sehemu ya kupanuka kwa kile ambacho ni wewe mwenyewe. Jinsi unavyojifunza zaidi kutiuni ndivyo zaidi Sauti itarejea.

Huenda ikawa kwamba Sauti itatokea wakati wewe uko nje unatembea. Ili mradi huhitaji kutembea kwenye barabara yenye magari au njia ngumu unaweza Kutahajudi wakati unatembea. Unachohitaji tu ni wewe kuunganisha na kuoanisha Sauti pamoja na hisia zako zingine za (kimwili). Hii sio ngumu kama inavyoonekana na kwa kufanya mazoezi kidogo itakuwa njia ya kawaida ya kuwa. Utakuwa na uwezo wa kuishi katika dunia na zaidi ya Dunia kwa wakati mmoja. Kuwa na ufahamu wa kuwa kwako kimwili na Kuwa Kiroho kwa wakati huo huo hakika ni njia ya kawaida na kiasili ya kuwa!

Zaidi ya hayo, unaweza kuona kwamba wewe unaanza kuona Mwanga unapofunga macho yako. Sisi hatumaanisha mwanga wa akili lakini kwa Mwanga wa Kiroho. Hii itachukua aina ya maumbo na rangi ambazo hukua wazi na kali kadri wewe unavyojifunza Kutahajudi zaidi. Kama kwenye Sauti jaribu kutochambua na kutochanganua kile unachoona. Angalia tu bila kuchunguza au upendeleo wowote na acha Mwanga uwepo tu.

Mara tu wewe utakapojaribu kuingiliana na Mwanga utatoweka. Jiruhusu mwenyewe kuwa macho na kuruhusu siri kufunuka kikawaida na kiasili. Nguvu hizi zitakuchukua kwenye Safari ya ajabu ambayo kuna uwezekano unaweza kuishia katika Enlightenment ya Kiroho!

Huenda ikawa kwamba unahitaji msaada. Kwa hali yoyote ile omba msaada kwa mmoja wa Watahajudi wetu ambao tayari wametembea Njia ya Tahajudi. Wana uwezo wa kuhamisha Nguvu na kufanya Safari yako rahisi kutembea.

Ukitaka kutuma barua pepe Bofya Hapa tu.