Ujumbe kutoka kwa Uongozi wa Kiroho

 

Watu wengi wanapokea Ujumbe kutoka Ngazi za Juu za Maumbile kwa wakati huu. Ngazi za juu za Kiroho zimejaa idadi kubwa ya Viumbe Inteligent ambao kila moja ana ajenda zao na malipo.

Njia ya Tahajudi ya Mwanga na Sauti ambayo tunazungumza inasimamiwa na Kikundi tunachokiita Uongozi wa Kiroho. Hili ni jina ambalo tumewapa. Tunafahamu kuwa wengi wao wamekuwa na maisha ya Kidunia na kwa hivyo wakati mwingine huitwa Mabwana waliopaa (Ascended Masters). Walakini, ili kuepukana na kughilibiwa na ego Wao karibu kila wakati wataficha kuwa wao kweli ni nani.

Wakati Mtahajudi anapokea Ujumbe huwa wakati mwingine hajui ni wapi ulitokea.


21 Juni 2020

Ni wazi kwamba utata utatokea wakati kuna mtiririko wa Ujumbe. Kwa sababu watu wanaweza kuwasiliana na Wajumbe wa aina nyingine katika Ngazi tofauti kuna uwezekano wa kuwa na mzozo, hata hivyo, sio kwa ubaya.

Hii ni kuelezea tu, kwamba unajua kila wakati ni kutoka kwetu wakati ujumbe ni rahisi na umeelezewa na kuonyeshwa tu na kwa mpangilio wa aina fulani.

Tumekuwa tukipokea ujumbe kwa zaidi ya miaka 5 na tunaweza kushuhudia, kabisa kwa haya hapo juu. Ingawa Ujumbe unaweza kuwa unatoka kwa Wajumbe tofauti wa Uongozi wa Kiroho au vikundi tofauti, Ujumbe wote una mtindo sawa. Ni ujumbe mfupi, wa kivitendo, wa moja kwa moja, rahisi, uliopangwa na zaidi ya yote wa Huruma na Upendo.

Swali: Tunaomba kuuliza ili ufafanue, kwa njia rahisi, ambacho tunakiita kama Uongozi wa Kiroho ili kuwa na ufafanuzi unapozungumza juu ya Viumbe wengine katika Ngazi tofauti.


24 Juni 2020

Ni swali zuri sana ambalo watu huuliza, kwa kuwa mambo yanakuwa na utata tunapoongea juu ya Ulimwengu Nyingi na viwango vingi vya Ufahamu na mengineyo.

Kuna Viumbe wengi wasio hesabika kama unavyojua, ambao wanakaa Ngazi za Juu. Ni wachache tu wanaovutiwa na Maswala ya Kidunia/KiSayari.

Kwa maneno rahisi sana, Uongozi wa Kiroho ambao unawasiliana nao, tangu mwanzo, mara zote walipendelea Mwanga na Sauti ya Kiroho katika mafundisho yao ya msingi.

Kuna Mantras bila shaka na mbinu za kujituliza za kutahajudi zote zinazoelekea kwenye Kuanzishwa ambako kunaonyesha mlango wa Ngazi za Kiroho. Halafu, wakati Mtahajudi anavyoendelea, Mwanga na Sauti zinamwongoza na kumfundisha njia nzima na kugundua kuwa kuna kitu kimoja tu kila Mahali na hicho ni Mungu.

Usomaji wote wa vitabu vya Kiroho hauwezi kukupa zawadi hiyo ya kushangaza – unahitaji kujionea mwenyewe.

Ni vizuri kuzingatia kuwa Mafundisho ya kimsingi ya Uongozi wa Kiroho ni yale ya Tahajudi ya Mwanga na Sauti. Ingawa matumizi ya mazoezi ya kutulia na Mantra yanaweza kuwa muhimu sana awali kwa kuandaa watu. Kusudi linapaswa kuwa kila wakati kufunua Nguvu za Kiroho za kweli ambazo zitakuza Ufahamu wa Mtahajudi na kuwaongoza kwenye Ukombozi wa Ufahamu au Enlightenment.


26 Juni 2020

Kuhusiana na Njia na Mbinu za taswira ya kuona (visualisation techniques), watu wengine hawako tayari kuja kwenye Njia ya Kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti mara moja. Wanahitaji kazi na maandalizi ili kuzoea kutahajudi na kuzoea kutulia.

Unajua kasi ya maisha katika ulimwengu mnaoishi – ni sawa kila-mahali.
Waache watu wafurahie taswira – inafanya maisha yao kuwa yenye furaha na kutosheleza.

Halafu, wakati wakiwa tayari, wengine, au labda wengi wao watakuja kuanzishwa – hakuna haraka na watakuwa tayari zaidi kujiachia kwenye Mwanga na Sauti, kwani wamezoea kuwa na utulivu.

Jambo la msingi, watu wanahitaji kujifunza jinsi ya kutulia na kujiachia. Sisi sote ni tofauti na hivyo tahajudi za kuongozwa zitafaa watu wengine wakati wengine watanufaika na mbinu za taswira (isualizing techniques). Mantra ni muhimu sana na zina nguvu ikiwa inatumiwa kwa usahihi. Mbinu hizi zote ni njia nzuri za kuwandaa watu kwa siku watakapoungana na Mwanga na Sauti na kuanza Safari yao ya Kiroho.