Ego

 
Kusudi la maisha ya mwanadamu ni mambo mawili, kupenda na kujifunza. Tunaendeshwa katika miaka yetu ya mwanzo na ego zetu; zinahitaji usikivu kwetu wenyewe na wale walio karibu yetu. Kwa maneno mengine sisi ni wabinafsi na tanafuta ubinafsi.

Hii ni kawaida na asili tu kwani tuna tamaa ya kuishi. Kwa watu ambao wanazaliwa katika mazingira magumu hii inaweza kuwa nguvu ya kuwaendesha ambayo inaongoza na kutawala maisha yao yote. Hata hivyo, kwa wengi wetu tunajifunza haraka sana jinsi ya kuwa hai na kushirikiana na familia zetu, marafiki na wafanyakazi wenzetu.

Tunajua kwamba tunaweza kutoa na kuwasaidia watu walio na bahati mbaya na kumsikiliza mtu ambaye anataka kutueleza matatizo yake. Kisha wakati huo uchaguzi unakuwepo; tuko hapa kujitumikia wenyewe au kuwatumikia wengine.

Wakati mtu anapokuwa na ufahamu wa Nguvu za Mwanga na Sauti wanatambua kuwa ule ubinafsi mdogo ni sehemu tu ya kile ambacho kweli ni wao – kama ncha ya barafu baharini! Wanagundua kwamba kwa Kweli wao ni Viumbe wa Kiroho ambao hukaa nyuma ya kile tunachokiita binadamu. Wanatambua kuwa Ngazi za juu za Kiroho ni kiellezo cha juu kuliko vyote cha Upendo wanapofanya kazi kupitia Utoaji kamili wa jumla – bila kuomba kitu chochote.

Hili sio imani, ni Elimu Kamili!

Swali sasa linabakia, “Mtu huyo afanyeje kueleleza Hali hii ya utakatifu?” Kwa sababu ilitolewa bure kwa uhuru hakuna vikwazo au mahitaji; mtu anaweza kuendelea na maisha yake kama ilivyokuwa kabla. Hata hivyo, sasa wana uwezo wa ajabu wa kuona ego yao kuwa ni nini – ndogo sana na yenye madai sana kila wakati.

Mtu kama huyo sasa ana nafasi ya kuipita nafsi yake ndogo na badala yake kujitolea maisha yake kwa juhudi zaidi, bila uchoyo, huruma na Upendo. Wanaweza kugeuza nguvu na usikivu wao ili kuwasaidia wengine. Hii inaweza kuwa kwa mambo ya kidunia au kuwasaidia watu kwa mambo ya Kiroho ili wao pia waweze kuwa na ufahamu wa Mwanga na Sauti.

Sisi kama wanadamu tuna uhuru wa nafsi (free will) kwa hiyo uchaguzi daima ni wetu!

Hii inatoka kwa Mabwana wa Mwanga, wakizungumzia kuhusu Ego

Ego ni moja ya changamoto tano ambazo mwanadamu anahitaji kukabiliana nazo. Zingine zikiwa Uchu, Hasira, Uchoyo na Kujishikamanisha. Wakati mwingine hujulikana kama Vidole Vitano vya Kifo. Bila Ego mwanadamu hawezi kuishi – inamaanisha ule ubinafsi au “Mimi”.

Lakini, kama ilivyo kwa kila kitu katika maisha inabidi kuwe na usawa. Unahitaji kuzingatia mambo yako na uhakikishe kuwa mahitaji yako ya kidunia na kimwili yanatoshelezwa.

Lakini kutokea pale ambapo tunaangalia Dunia na wakazi wake hivi sasa tunaweza kuona kwamba hisia ya Ego imeenea sana katika maisha ya watu wengi. Tunapaswa kusema kwamba hata watu ambao wanaweza kujihesabu kuwa wa Kiroho wanaweza kuwa wachoyo na wabinafsi.

Hii ina athari mbaya kwenye usawa wa Dunia na inahitaji kushughulikiwa. Wakati Ego ni nje ya usawa huharibu hisia ya amani na ustawi kwa mtu, swala ni kuhakikisha kwamba unatilia maanani umuhimu wa watu wengine. Hiyo ndivyo jamii inavyofanya kazi vizuri na kila mmoja jinsi anavyoweza kuonyesha hali yao ya Kiroho na upendo wa kiasili kwa Dunia.