Kutoka kwa Uongozi wa Kiroho imeandikwa sawa kama ilivyopokelewa.
Tumeshaelezea kuwa Upendo ni kanuni ambayo inazunguka kila kitu na kila kitu kipo kwa sababu yake. Ikiwa hivyo ndivyo ilivyo kwa nini kuna vita vingi duniani? Je! Hii haiendi kinyume cha asili ya mtu? Kwa nini inakuwa kwamba katika dunia ambayo ipo kwa sababu ya Upendo kunaweza kuwa na chuki sana kiasi hiki?
Jibu liko katika ‟duality”. Ndani na nje, nzuri na mbaya, juu na chini, upendo na chuki. Kazi ya Mwanadamu ni kuvuka zaidi ya asili yake ya ‟duality” hapa duniani, kutahajudi kwenye Mwanga na Sauti ambayo itamwonyesha njia ya kutafuta Upendo kwenye Enlightenment ambao hauna kinyume.
Upendo upo wenyewe, hauna masharti, bila mwisho, bila mipaka.
Hakuna hukumu kwenye Upendo.
Upendo ni msamaha na hauhitaji……… (Waliacha hapa wazi; tunafikiria wanataka sisi tujaze!)
Upendo unakubali kila kitu kama kilivyo.
Upendo unaopatikana kwenye Enlightenment ni Safi, haujachafuka na hauwezi kuathiriwa.
Upendo uko daima.
Furaha ya kweli ni Upendo wa milele.
Upendo ni kielelezo cha mwisho cha Kweli. Haikatai chochote na huzidi kila kitu.
Kuna uzuri gani zaidi kuliko Upendo uliopatikana kwenye Enlightenment?
Upendo ndiyo kitu pekee ambacho hakiwezi kudhibitiwa. Upendo una kila kitu; Upendo ni tegemezo la kila kitu.
Upendo ni kielelezo cha Mwisho cha Umoja wa Ulimwengu wote.