Maisha au Safari ya Nafsi

 
Makala yafuatayo ni katika kurahisisha mafudisho tuliyopokea hivi karibuni kutoka kwa Uongozi wa Kiroho

Kwanza tunahitaji kufafanua baadhi ya maneno:
Kiini – Kile ambacho kweli ni Wewe na daima kinaendelea kubaki kwenye Ngazi au Ulimwengu wa Kiroho.
Nafsi – Sehemu ya Kiini ambayo inachukuwa mwili.

Wakati nafsi iko karibu kuchukua mwili Kiini au kile ambacho kweli ni Wewe hutayarisha mpango mahsusi wa maisha yale, pamoja na Idadi ya Viumbe wa Kiroho wakiwa kama washauri. Madhumuni ya safari ya maisha yanatayarishwa vyema na mazingira ya kuzaliwa yanachaguliwa kwa uangalifu mkubwa. Zingatio si tu kwa eneo la sayari pekee bali pia wanafamilia, marafiki na hata watu ambao watakuwa na ushawishi katika maisha hayo. Miili (ya kimwili, kihisia na kiakili) nayo pia inachaguliwa kudhihirisha maisha yaliyochaguliwa. Hivyo basi wewe ni “Mkono ulioko ndani ya glavu (glove)” na ni “Mkono“ huu unaoufahamu au unaofunuliwa wakati unaanzishwa katika safari ya Mwanga na Sauti.

Ziada na mpango wa maisha, kila mtu “anagawiwa” idadi ya “vibambo egemezi” (“wildcards”) ambavyo vinawajibika na kile tunachokiita utashi huru (free will). Hivi vitasababishi tuache kufuata mpango wetu wa maisha na pengine kwenda nje ya mstari na yawezekana matokeo yakawa aidha mazuri au mabaya. Na hapa ndipo Karma inapokuja katika “Mlimgano” na hali kuwa mtafaruku kweli. Tunaambiwa kwamba namna pekee ya kukabiliana au kupata “Karma” ni pale unapocheza na kutumia “ vibambo egemezi”. Kama ukifuata mpango wa maisha uliopangwa huwezi kupata Karma kwani unacheza mchezo na kufuata maelekezo uliyopewa.

Wakati wa uhai, mtu atajaribu kujifunza seti za masomo, yawezekana yakawa mafunzo ya kitaaluma na hali kadhalika ya kimaisha. Sisi kamwe hatuachi kuwa na fursa ya kujifunza. Kama tatizo fulani likiendelea kujitokeza, ni ishara ya wazi kabisa kwamba tumeshindwa kulishughulikia ipasavyo; kinyume chake “tunalifunika”. Na kama funzo liko pale basi tunapaswa kukabiliana na changamoto vyema, zaidi ya yote, sisi wenyewe ndio tumelipanga somo au funzo!

Tunapokufa, inatumainika kuwa tutakuwa tumejifunza mengi ya masomo yetu, vinginevyo tutahitaji kuyaingiza na kuyajumuisha kunako maisha yetu yajayo. Katika kifo cha kimwili tunapaa kwenda kwenye Ngazi za Kiroho lakini bado tunaendelea kushikilia miili yetu ya kihisia na kiakili. Kwenye Ngazi hizi tunaumba uzoefu wetu wa “Peponi au Mbinguni” lakini hatimaye unafika wakati ambapo miili yetu ya kihisia na kiakili nayo pia lazima iachiwe.

Hapo ndipo tunapoingia katika kipindi cha mapumziko na tafakari kabla ya kujiunga tena na Kiini chetu ambacho chenyewe kinaendelea kujifunza.

Kama ilivyoelezwa hapo juu, huu ni kama mfano mwepesi lakini unaoonyesha baadhi ya taratibu ngumu na pana zaidi wakati Nafsi inachukua mwili.

Kama una swali lolote tafadhali jisikie huru kuuliza kupitia ukurasa wa mawasiliano. Jaribu kuyafanya yawe kwa upana badala ya kukuhusu wewe pekee, hivi kwamba tuweze kuyatuma na kuyaweka kwenye totvuti.