Upendo

 

Upendo ni Nguvu isiyo na mipaka ambayo inazunguka Uumbaji wote. Mahali popote unapoangalia kuna Upendo, kwa sababu kila kitu ambacho unaweza kuona, kuhisi na kugusa kipo kwa sababu yake. Kila kitu kimeunganika, hivyo kila wazo, tendo au neno linarekodiwa.

Hakuna kitu kinachopotea: maneno yaliyosemwa kwa hasira yana nguvu zaidi na husababisha uharibifu zaidi hivyo jaribu kuwa mpole zaidi katika ufanyaji na mtazamo wako wa mambo. Dhibiti hisia zako kwa kuangalia na kufikiria kabla ya kuzungumza.