‟Ascension” Itaanza lini?

 

Tunaelewa kutoka kwa Uongozi wa Kiroho kwamba ‟Ascension” haitakuwa tukio la janga lakini mchakato wa taratibu na upole.

Watu wanavyoanzishwa zaidi na zaidi kwenye Nguvu za Mwanga na Sauti zitaanza kuwa na ongezeko la athari nzuri kwenye Sayari hii na ni wakazi wake. Utaratibu na mchakato huu umeanza na kuna ishara nyingi zinazoonyesha hili.

Tumeelezea kuwa watu ulimwenguni pote wanakuwa na ufahamu wa sauti za juu. Wengi wanafikiri ni kawaida na kila mtu anajua; wengine wanafikiri ni hali ya matibabu kama vile “tinnitus”! Ukweli ni kwamba watu wanakuwa nyeti zaidi na wana”sikia” kwa njia tofauti. Sauti tunayozungumza haisikiki kwa masikio ya kimwili. Ni kama vile hisia nyingine imepatikana! Huu ndio Mtiririko wa Sauti ambayo Watahajudii wenye uzoefu wanaizungumzia na imeandikwa vizuri katika vitabu vya Kiroho. Jambo la kushangaza ni kwamba watu wengi ambao wanaripoti jambo hili hawajawahi kutahajudi katika maisha yao.

Watu wengine wanakuwa na ufahamu na Mwanga. Hii kawaida inachukuwa aina ya maumbo ya kijiometri na rangi. Asili yake sio ya kimwili; inaonekana wakati uko macho kamili na macho yamefungwa hasa katika chumba chenye giza. Sio aina ya kuota ukiwa macho au kutengenezwa kwa kutumia mawazo. Wale wanaoshuhudia hii Nishati wanaripoti kuwa ina ubora wa kinga na Upendo. Watu ambao wanaona huu Mwanga pia husikia Sauti.

Asili inaonekana “kuamka”. Watu wanaisikia ndege wanaimba zaidi mwaka huu na inaonekana kwa sauti kubwa na mara kwa mara. Kama ndege wanabadilika au kama watu wanakuwa nyeti na hisia zaidi hatujui. Tunachojua ni kwamba jambo hili limeripotiwa kutoka duniani kote kuanzia mapema mwaka 2017.

Sehemu nyingine ya mabadiliko inaonekana inaendelea wakati wa usingizi. Watu wanaripoti kuwa na ndoto nzuri na kwa uwazi zaidi na inaweza tu kuelezewa kama maisha sambamba. Kuwepo huku mbadala ni halisi kama vile maisha ya duniani. Ingawaje mandhari ni ya kawaida upitaji wa muda na wakati na sheria za fizikia ni tofauti kabisa.

Matukio mengi yaliyo orodheshwa hapo juu yanatokea kwa vijana, wengi wao kati ya miaka kumi na tatu hadi kumi na tisa. Wao wanakabiliwa na shida ya kukejeliwa na wenzao na/au kuitwa watu wa ajabu na kuweka chini ya huduma ya kiakili na wazazi wao. Kwa sababu hizi hubaki kimya na kuweka kila kitu kuwa siri yao wenyewe. Ni muhimu tuwahimize kuongea. Sisi kama Watahajudi wa Mwanga na Sauti tunajua kwamba Ulimwengu una Maajabu mengi na tunaweza kuwahamasisha na kuwapa msukumo wale walio karibu nasi kuzungumza juu ya Kweli.

Uongozi umeelezea kwamba ‟Ascension” italeta uelewa zaidi ambao utasaidia kuongeza maelewano kati ya wakazi wa Sayari hii. Hasa vijana “wataamka” kwa mabadiliko haya na kuwa na Ufahamu zaidi; hatimaye hatma ya Dunia iko mikononi mwao.