“Ascension” Imeanza

 
Tunaelewa kutoka Uongozi wa Kiroho kwamba Ascension haitakuwa tukio la ghafla lakini taratibu na mchakato laini na wa polepole.

Jinsi watu zaidi na zaidi wanavyoanzishwa, Nugvu za Mwanga na Sauti zitaanza kuwa na athari nzuri zaidi kwenye Sayari hii na wakazi wake. Mchakato tayari umeanza na kuna dalili nyingi zinazoonyesha hii.

Sisi tayari tulishataja kwamba watu Duniani kote wanakuwa na ufahamu wa Sauti ya juu. Wengi wanafikiria ni kawaida na kila mtu anaisikia; wengine wanafikiri ni hali ya utabibu kama vile tinnitus! Ukweli ni kwamba watu wanaendelea kuwa nyeti zaidi na “kusikia” kwa njia tofauti. Sauti tunazozisema hazisikiki kwa masikio ya kimwili. Ni kana kwamba hisia nyingine zimepatikana! Hii ndiyo Mtiririko wa Sauti ambayo Watahajudi wazoefu wanaisema na imeandikwa vizuri katika vitabu vya Kiroho. Jambo la kushangaza ni kwamba idadi kubwa ya watu wanaoripoti matukio haya hawajawahi kutahajudi katika maisha yao.

Baadhi ya watu wanakuwa na ufahamu wa Mwanga. Hii kwa kawaida huchukua mfumo wa maumbo ya kijiometri na rangi. Sio ya kimwili katika asili; huonekana wakati ukiwa macho kikamilifu na macho yamefungwa hasa wakati ukiwa katika chumba chenye giza. Si aina ya ndoto au fikira iliyoundwa kwa kutumia mawazo. Wale wanaoshuhudia Nguvu hii wanapoti kuwa ina ubora wa kinga na Upendo. Watu ambao wanaona Mwanga bila kutofautiana pia husikia Sauti.

Asili inaonekana kuwa “inaamka”. Watu wanasikia “Sauti ya Ndege” zaidi mwaka huu na inaonekana kubwa zaidi na mara kwa mara. Kama ndege wanabadilika au kama watu wanaendelea kuwa na hisia zaidi hatuna uhakika. Tunachojua ni kwamba jambo hili limeripotiwa kutoka pande zote Duniani na limeanza mapema mwaka 2017.

Sehemu nyingine ya mabadiliko inaonekana kuwa hutokea wakati wa kulala. Watu wanaripoti kuwa na ndoto za uwazi zaidi kitu ambacho kinaweza kuelezewa kama maisha sambamba. Huku Kuwa au maisha mbadala ni kama kweli na kama yale maisha yao ya Duniani. Wakati mandhari ni ya kawaida jinsi muda unavyopita na sheria za fizikia ni tofauti kabisa.

Mengi ya matukio yaliyotajwa hapo juu hutokea kwa vijana, ambao wengi wao ni umri kati ya kumi na tatu mpaka kumi na tisa. Wao wanakabiliwa na matatizo ya kejeli toka kwa wenzao na/au kuitwa watu wa ajabu na kuwekwa chini ya uangalizi kwenye hospitali za wagonjwa wa akili na wazazi wao. Kwa sababu hizi wao hukaa kimya na kukaa na siri zao wenyewe. Ni muhimu kwamba sisi tunawahimiza kuzungumza. Sisi kama Watahajudi wa Mwanga na Sauti tunajua kwamba Ulimwengu umejaa Maajabu na tunaweza kuwahamasisha wale walio karibu yetu kuzungumza kuhusu Kweli.

Uongozi wa Kiroho wametuambia kuwa Ascension italeta unyeti zaidi ambao utasaidia kuongeza maelewano kati ya wakazi wa Sayari hii. Hasa vizazi vipya vita”amka” kwa mabadiliko haya na kuwa Ufahamu zaidi; hatima ya dunia hatimaye itakuwa kwenye mikono yao.